Neymar afikisha bao la 100 la mashindano kombe la dunia mwaka huu.
Baada jana Brazil kuibuka na ushindi wa mbao 4-1 dhidi ya Cameroon,Mchezaji Neymar alifunga mabao mawili na bao lake la kwanza limekamilisha mabao 100 yaliyofungwa ndani ya michuano ya kombe la dunia Brazil 2014.Brazil ni timu pekee iliyofunga bao la 100 katika mashindano husika mbali na Ujerumani. Mashindano ya mwaka huu yameonekana kuwa na mabao mengi kwani mpaka sasa kila mechi kuna wastani ya mabao 2.97 kila mechi ikilinganishwa na yale ya mwaka 1970.
Neymar kwa sasa amefikisha mabao 4 katika michuano ya mwaka huu mbele ya Thomas Muller (Ujerumani ), Robin Van Persie, Robben (Uholanzi), Karim Benzema (Ufaransa) pamoja na E Valencia (wa Ecuador) ambao wana mabao 3 kila mmoja.
0 comments:
Post a Comment