Friday, 20 June 2014

Kesho ndugu wawili Boateng kupambana tena kombe la dunia

Wakati leo hii Italia ikijiandaa kupepetana na Costarica , Kevin-Prince Boateng na Jerome Boateng ambao ni ndugu kesho (Jumamosi ) watakutana uso kwa uso kwenye Mechi ya Kundi G la Fainali za Kombe la Dunia huko Estadio Castelão Mjini Fortaleza, Brazil.
Siku hiyo, Ghana itaivaa Ujerumani kwenye Mechi zao za Pili za Kundi G huku Ghana wakiwania ushindi baada ya kufungwa Mechi yao ya kwanza na Marekani mabao 2-1 na Ujerumani ikitaka kuendeleza ushindi baada ya kuichapa Ureno mabao 4-0.
Kevin-Prince Boateng, anaechezea Ghana, ameeleza pambano hilo litakuwa la ‘kufa na kupona’ wakati atakapokabiliana na Ndugu yake Jerome Boateng anaechezea Ujerumani.
Mwaka 2010, huko Afrika Kusini, kwenye Fainali za Kombe la Dunia, Kevin-Prince na Jerome, walivaana wakati Nchi zao zilipokutana na kuweka Historia ya kuwa Ndugu wa kwanza kabisa kuchezea Timu pinzani.
JUMAMOSI, JUNI 21, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Argentina v Iran
F
Estadio Mineirão
2200
Germany v Ghana
G
Estadio Castelão
0100
Nigeria v Bosnia-Herzegovina
F
Arena Pantanal

0 comments:

Post a Comment