Sijiuzulu-Hodgson
Kocha wa Uingereza Roy Hodgson amesema hana nia ya kujiuzulu licha ya Timu yake kuchungulia kutupwa nje baada ya kufungwa Mechi yao ya Pili ya Kundi D la Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil.
Jana, mabao mawili ya Luis Suarez, anayecheza Liverpool, yaliwaua Uingereza mabao 2-1 katika Mechi yao ya Pili ya Kundi D.
Kwenye Mechi ya Kwanza Uingereza walipigwa 2-1 na Italy.
Wayne Rooney
ndiye aliefunga Bao la England na kufunga midomo ya Watu waliokuwa
wakimpinga na sasa hao hao wakingojewa kusema kama watamnanga Steven
Gerrard ambaye ndiye alitoa upenyo kwa mwenzake wa Liverpool Suarez
kufunga Bao la ushindi.
Ikiwa Leo Italy na Costa Rica
zitatoka Sare basi Uingereza wako nje lakini matokeo mengine yanawapa
nafasi Uingereza ikiwa wataifunga Costa Rica kwenye Mechi ya mwisho na
Matokeo mengine kwenda kwao.
Lakini kocha wa England, Roy Hodgson, amekata kujiuzulu na kuiacha FA iamue inachotaka.
0 comments:
Post a Comment