Klabu bingwa Afrika TP Mazembe na Zamalek leo jumapili,Etoile yashinda kwa taabu
Klabu ya Etoile du Sahel jumamosi hii ilitoka nyuma na kushinda mabao 4-3 dhidi ya Nkana ya Zambia katika mashindano ya kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka 2014 na kupanda kileleni mwa kundi la B.Mabingwa hao wa mwaka 2006 wamefikisha alama 5 moja zaidi ya Al Ahly.
Matokeo mengine hiyo jana ni kwamba Asec Mimosas kutoka Ivorycoast ilikibali kichapo cha mabao 3-2 dhidi ya Coton Sport ya Cameroon.
Sewe Sports itacheza leo jumapili na AL Ahly kutoka Misri na AS Real de Bamako itacheza na AC Leopards de Dolisie
Kwa upande wa klabu Bingwa yaani CAF CHAMPIONZ LIGI TP Mazembe, yenye Wachezaji mahiri wa Tanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, itakuwa Nyumbani Lubumbashi kuwavaa Wakongwe wa Misri Al Zamalek.
Jumapili Juni 8
TP Mazembe v Al Zamalek
Espérance Sportive de Tunis v Club Sportif Sfaxien
0 comments:
Post a Comment