Sunday, 8 June 2014

Pigo kwa Nigeria Echiejile kukosa kombe la dunia 2014

Beki wa Nigeria  Elderson Echiejile atakosa fainali za kombe la dunia kwa sababu ya maumivu ya msuli.
Mchezaji huyo mwenye miaka 26 anayechezea klabu ya  Monaco  aliumizwa katika suluhu ya   0-0 Nigeria ikicheza na Ugiriki katika mchezo wa kujipima nguvu.
Echiejile baada ya kufanyiwa uchunguzi amebainika kuwa atakaa nje ya dimba kwa wiki 3
Nafasi yake itachukuliwa na winga wa  Enugu Rangers anayeitwa  Ejike Uzoenyi.
Kocha  Stephen Keshi alisema: "dakatari amsema  Echiejile anahitaji wiki tatau ili apone,hatuna muda wa kusubiri ili apone,tumeamua kumchukua mchezaji mwingine ."
Nigeria itapambana na  Iran, Bosnia-Herzegovina na  Argentina katika kundi la  F, wataanza na  Iran katika uwanja wa  Curitiba Juni 16 .
Kikosi cha Nigeria:
Makipa: Vincent Enyeama (Lille), Austin Ejide (Hapoel Be'er Sheva), Chigozie Agbim (Gombe United).
Walinzi: Efe Ambrose (Celtic), Godfrey Oboabona (Rizespor), Azubuike Egwuekwe (Warri Wolves), Kenneth Omeruo (Middlesbrough), Juwon Oshaniwa (Ashdod), Joseph Yobo (Norwich, mkopo kutoka Fenerbahce), Kunle Odunlami (Sunshine Stars).
Viungo: John Mikel Obi (Chelsea), Ramon Azeez (Almeria), Ogenyi Onazi (Lazio), Reuben Gabriel (Waasland-Beveren), Michael Babatunde (Volyn Lutsk), Ejike Uzoenyi (Enugu Rangers).
Washambuliaji: Ahmed Musa (CSKA Moscow), Shola Ameobi (Newcastle), Emmanuel Emenike (Fenerbahce), Michael Uchebo (Cercle Brugge), Peter Odemwingie (Stoke), Victor Moses (Liverpool, on loan from Chelsea), Uche Nwofor (Heerenveen).

0 comments:

Post a Comment