Mbio za kugombea tuzo ya mfungaji bora kombe la dunia
Wakati fainali za kombe la dunia zikiwa zimeanza mechi zake za mwisho kwa upande wa makundi,baadhi ya wachezaji wameshaingia kwenye list ya wanaowania tuzo za mfungaji bora kwa upande wa mabao.Hawa ni baadhi tu ya wale ambao wameonekana kufunga mabao mengi kwa sasa mwaka 2014 kule Brazil.
Neymar da Silva (Brazil) jana alifunga mabao mawili kati ya manne baada ya Brazil kushinda mabao 4-1 dhidi ya Camerron amefikisha jumla ya mabao manne na kwenye listi yeye ndiye anaongoza.
Wachezaji ambao wana mabao 3 kila moja ni
Thomas Muller (Ujerumani ), Robin Van Persie, Robben (Uholanzi), Karim Benzema (Ufaransa) pamoja na E Valencia (wa Ecuador) .
Wachezaji wenye mabao mawili ni pamoja na Lionel Messi (Argentina), Tim Cahill (Australia), Mario Mandzukic (Croatia), LUIS Suarez (Uruguay), Gervinho (Ivory Coast), Rodriguez (Colombia), Dempsey (USA), A Ayew (Ghana).
Baada ya Australia kufungashwa virago Tim Cahill wa nchi hiyo atabaki na mabao hayo pia Mario
Mandzukic (Croatia) timu yake imekwishatolewa kwa hiyo atabaki na mabao yake mawili.
Wachezaji Rodriguez,Suarez wakifunga hii leo watajiongezea hazina ya mabao katika fainali hizi ambapo mpaka jana tayari mabao 108 yamekwishafungwa.
JUMANNE, JUNI 24, 2014 | |||
SAA | MECHI | KUNDI | UWANJA |
1900 | Italy v Uruguay | D | Estadio das Dunas |
1900 | Costa Rica v England | D | Estadio Mineirão |
2300 | Japan v Colombia | C | Arena Pantanal |
2300 | Greece v Ivory Coast | C | Estadio Castelão |
0 comments:
Post a Comment