Wednesday, 18 June 2014

Mtangazaji wa radio moja Tabora akumbana na changamoto ya ratiba kombe la dunia

Wakati michuano ya kombe la dunia ikiendelea kurindima kule nchini Brazil,ratiba imekuwa changamoto kubwa ambapo kuna baadhi ya watu huchanganya muda wa Brazil na Tanzania lakini wengine wakishindwa kuwahi majukumu yao asubuhi kutokana na baadhi ya michezo kupigwa usiku.
Mtangazaji maarufu mkoani Tabora mbaye anafanya kazi kwenye redio moja kubwa anakumbana na changamoto  kwani anashindwa kuwahi vipindi vya asubuhi kutokana na kukodolea macho kwenye runinga akishuhudia michezo ya kombe la dunia mpaka usiku wa manane.
Mtangazaji huyo mwenye mbwembwe nyingi akiwa redioni anafanya kipindi cha jamii ambacho hupendwa kusikilizwa na wanajamii amesema amefanya kazi kwenye redio kwa  zaidi ya miaka minne na fainali zilizopita  kule Afrika kusini alishuhudia vema lakini michuano ya mwaka huu yamekuwa changamoto kwake.
Mtangazaji huyo ambaye ameonekana yuko makini na Ratiba ya kombe la dunia amesisitiza kuwa ataendelea kushuhidia michezo hiyo hadi mwisho ingawa kuchelewa kwake hakutaathiri kipindi chake ambacho kinapendwa na watu wa kanda ya magharibi.
Mapema wiki hii mwanahabari huyo alichelewa kuwahi kazini kwake kwa muda aliojiwekea na kuchelewa kwa dakika 5 ingawa aliingia kwenye kipindi na kufanya kwa ueledi mkubwa.

Wakati hayo yakiendelea mashabiki pia wamelalamikia ratiba ya michezo ya mwaka huu.
Wakizungumza na Sports4lifetz mashabiki wawili mkoani Arusha wamesema kuwa imekuwa tatizo kwao kukosa baadhi ya michezo kutokana na ratiba kutoeleweka kwao,mmoja wa mashabiki hao jina linahifadhiwa amesema kuwa wakati anasubiria mchezo kati ya Uingereza na Italia ambao ulipigwa majira ya saa saba usiku yeye alifikiri mchezo ni saa saba mchana.

Mshabiki mwingine ameeleza kuwa mchezo kati ya Ivorycoast na Japan ambao ulipigwa jumamosi iliyopita majira ya saa kumi kuamkia asubuhi ulimpa wakati mgumu kwani kwa ratiba yake aliyojiwekea alidhani mchezo ni saa kumi jioni.
Michezo hiyo ambayo imeingia siku ya 7 itashuhudia leo majira ya saa moja kamili jioni Australia ikicheza na Uholanzi wakati saa nne kamili Usiku Hispania iliyodhalilishwa na Uholanzi itacheza na Chile wakati saa saba usiku Cameroon itashuka dimbani kucheza na Croatia.





0 comments:

Post a Comment