Wednesday, 18 June 2014

Matokeo ya jana na Ratiba ya leo kombe la dunia.

Mechi za Pili kwa Kundi A la Fainali za Kombe la Dunia zimeanza  Estadio Castelão, Fortaleza na Wenyeji Brazil kutoka suluhu kwa maana ya  0-0.
Suluhu hii imeibakisha Brazil juu kwenye Kundi wakiwa na alma 4 sawa na Mexico.
Wakati Kipindi cha Kwanza kilikuwa vuta ni kuvute ingawa Neymar alikosa Bao la Kichwa ambacho Kipa Ochoa aliokoa vizuri, Kipindi cha Pili Brazil,walikuja juu na kukosa mabao kadhaa huku Kipa Ochoa akiokoa mabao mengi na  aliinusuru Mexico.
Wakati  Mechi ya Kundi F iliyochezwa Arena Pantanal, Cuiba kati ya Urusi na Korea  Kusini ilimalizika kwa sare ya 1-1.
Korea walitangu;ia kufunga katika Dakika ya 68 kwa Bao la Lee Keun-ho na Mapema Jana, kwenye Mechi ya kwanza ya Kundi F, Ubelgiji iliifunga Algeria 2-1.
Jumatano ni zamu ya Cameroon na Croatia kucheza Mechi zao za Pili za Kundi A baada ya wote kupoteza Mechi zao za kwanza.
Mechi ya mwisho Brazil watacheza na Cameroon huko Nacional, Brasilia Jumatatu Juni 23 na wakati huo huo Mexico kuivaa Croatia.
 Ratiba ya leo
JUMATANO, JUNI 18, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Australia v Netherlands
B
Estadio Beira-Rio
2200
Spain v Chile
B
Estadio do Maracanã
0100
Cameroon v Croatia
A
Arena Amazonia

0 comments:

Post a Comment