Monday, 9 June 2014

Nadal abeba taji la French Open,akiri Djockovic ni mkali.

Nadal na Djockovic wakipeana mikono.
Rafael Nadal alifurahi baada ya jana  kuchukua ubingwa wa tisa wa michuano ya wazi ya Ufaransa na kusahau yaliyotokea kule Australia baada ya  kutoka mikono mitupu katika michezo ya wazi ya Australia  mapema mwaka huu.Nadal alifanikiwa kubeba taji hilo baada ya kumfunga Novak Djokovic katika fainali.
Djokovic  alikuwa anapewa nafasi ya kuwa  mtu wa nane kuchukua ubingwa mara nne japokuwa alishinda seti ya kwanza,Nadal  alikuja juu na kushinda  3-6 7-5 6-2 6-4.
Mhispania huyo anakuwa mtu wa kwanza kushinda mataji tano ya Wazi ya Ufaransa na kuweka rekodi zaidi katika michezo 66  alizoshinda kule Paris  kati ya  67 alizocheza.
Ushindi huo unamfanya Nadal aendelea kuwa nambari moja katika viwango vya tennis duniani.
Baada ya kumalizika kwa mchezo huo Nadal alikiri kuwa kabla ya mchezo huo alikuwa anamhofia Mpinzani wake lakini alishinda huku akisistiza kuwa amecheza naye michezo minne ya mwisho lakini alishindwa kabisa kumshinda mpinzani wake huyo.
Djokovic alimuajiri  Boris Becker ili awe kocha wake mkuu.

0 comments:

Post a Comment