Monday, 9 June 2014

TP Mazembe kidedea mbele ya Zamalek,Esparance wameshinda ila bado wapo mkiani

Rainford Kalaba
Ligi ya mabingwa barani Afrika imeendelea tena jana ambapo Klabu ya Tout Puissant Mazembe ya Congo DR ikiwa katika  Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi ilishinda bao 1-0 dhidi ya Zamalek ya Misri.
Goli pekee la ushindi lilifungwa na Rainfrod Kalaba dakika ya 13.
Mazembe sasa wanapanda kileleni baada ya kufikisha alama sita kutokana na mechi zote tatu za mzunguko wa kwanza.
Katika mechi zake mbili za kwanza, Mazembe ilifungwa 1-0 na El Hilal ya Sudan kabla ya kushinda 1-0 dhidi ya ndugu zao, As Vita ya Kinshasa, DRC .
Baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na AS Vita wikiendi hii, Hilal inafungana kila kitu na timu hiyo ya DRC, alama nne na wastani sawa wa mabao ya kufunga na kufungwa, kila timu imefunga mabao matatu na kufungwa matatu.
Zamalek inamaliza mkiani mwa kundi hilo kwaalama zake tatu.
Katika mchezo mwingine kundi la B hiyo jana ndugu wawili wa Tunisia walicheza ambapo Esperance ilishinda 2-1 dhidi ya Sfaxien.
Msimamo kundi la A                                                                                                                   Alama

1TP Mazembe (Congo DR)






6
2Al Hilal (Sudan)






4
3AS Vita (Congo DR)






4
4Zamalek (Egypt)






3


Kundi la B                                                                                                                                    Alama

1ES Setif (Algeria)





5
2CS Sfaxien (Tunisia)






4
3Al Ahly Benghazi (Libya)






4
4Esperance (Tunisia)






3

Mzunguko wa pili wa Ligi ya Mabingwa unatarajiwa kuanza baada ya Kombe la Dunia Julai.

0 comments:

Post a Comment