Thursday, 19 June 2014

Ruvu Shooting yaendelea kunasa vifaa,yamnasa wa Mtibwa

Kikosi cha Ruvu msimu uliopita.
Katika kujiimarisha kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu soka ya Tanzania bara kwa msimu wa 2014/2015,klabu ya Ruvu Shooting imeendelea kuibomoa klabu ya Mtibwa Sukari kwa kumsajili mchezaji Yusuph Mguya.
Taarifa iliyotumwa asubuhi ya leo kwenda Sports4lifetz na msemaji wa klabu hiyo Masau Bwire imeeleza kuwa Yusuph Mguya amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Ruvu Shooting.
Mapema mwezi uliopita mchezaji Juma Mpakala alisajiliwa na klabu hiyo akitokea Mtibwa Sukari ambapo alicheza tangu mwaka 2008 hadi msimu huu, pia  kiungo huyo mshambuliaji, aliwahi kuichezea Ashanti United msimu wa 2007/8.
Mpakala alisajiliwa sambamba na  Chagu Chagula,  Chagula ni mshambualiji wa Kitanzania aliyekuwa akiichezea timu ya Muzinga ya Burundi na kabla ya kwenda Burundi, aliwahi kucheza katika timu za Twiga, Kahama United na Ashanti United hadi mwaka 2007 alipotimkia nchini humo na kujiunga na timu ya Vital'O aliyoitumikia hadi 2009 mnamo mwaka 2010 hadi 2011 Chagula aliichezea timu ya Inter Star ya Burundi kabla ya kujiunga na Muzinga 2012 ambayo ameitumkia hadi msimu huu mkataba wake ulipomalizika..
Zuberi Dabi ndiye mchezaji wa kwanza kunaswa msimu huu akitokea Kagera Sukari.
Masau Bwire alishawahi kukaririwa akisema kuwa Kwa mujibu wa ripoti na mapendekezo ya kocha Olaba,wanabakisha kusajili mchezaji mmoja, beki wa kati na kueleza kuwa watafanya usajili makini ili watwae taji la Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao.
Ikumbukwe kuwa  Ruvu Shooting ilimaliza ligi kuu msimu uliopita ikiwa nafasi ya nne nyuma ya Azam,Yanga,Mbeya city na Simba kwa kujikusanyia alama 38.

0 comments:

Post a Comment