BFT yakamilisha leseni za mabondia
Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), limekabidhi leseni za mabondia watakaoshiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola nchini Scotland, kwa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC).Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga, alisema tayari wamekabidhi leseni za mabondia wote, hivyo wana uhakika timu kwenda kushiriki mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kuanza Julai 23 hadi Agosti 3.
Alisema TOC waliwataka viongozi wa BFT kupeleka majina hayo kabla ya wachezaji wote kurejea nchini ili waweze kufanya maandalizi ya ushiriki mapema.
“Tayari tumekabidhi leseni za mabondia TOC wiki iliyopita, hatuna deni tena kuhusu hilo, mabondia wote wapo vizuri China wanakojinoa kwa ajili ya mashindano hayo na tuna uhakika watapeperusha vema bendera ya taifa,” alisema.
Mashaga alisema bado wanaendelea na mazungumzo na kocha ambaye ataongozana na mabondia hao Scotland, katika mashindano hayo na kwamba wakikamilisha wataweka wazi.
Chanzo;Tanzania Daima.
0 comments:
Post a Comment