Simba sasa kuendelea na uchaguzi
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kupokea na kuzingatia maombi ya Simba, na kwa kuzingatia Ibara ya 26 ya Kanuni za Uchaguzi za TFF toleo la 2013 limeiruhusu klabu hiyo kuendelea na mchakato wa uchaguzi wao uliopangwa kufanyika Juni 29 mwaka huu.Taarifa ya TFF imesema kwamba inawahimiza wanachama wa klabu ya Simba kuwa watulivu na wafanye uchaguzi wao kwa amani.
Ikumbukwe TFF ilisimamisha mchakato wa uchaguzi wa Simba SC hadi hapo klabu hiyo itakapounda Kamati ya Maadili ambayo itasikiliza masuala ya kimaadili kuelekea uchaguzi huo.
Malinzi alisema mwishoni mwa wiki kwamba Simba SC inatakiwa kuwa imekwishaunda Kamati ya Maadili hadi kufika Juni 30, mwaka huu, hatua ambayo alidai imefuatia TFF kupokea malalamiko mengi juu ya ukiukwaji wa maadili kwa baadhi ya wagombea na wanachama wa klabu hiyo.
Malinzi alisema kwamba baada ya kuundwa kwa Kamati hiyo Maadili itasikiliza malalamiko yote ya kimaadili yanayougubika mchakato wa udhaguzi huo, ambao ulipangwa kufanyika Juni 29, mwaka huu.
Aliagiza Kamati ya Utendaji ya Simba SC iliyopo madarakani chini ya Mwenyeiiti wake, Rage iendelea kuiongoza klabu hiyo hadi hapo mchakato wa uchaguzi utakapokamilika.
0 comments:
Post a Comment