Sunday, 22 June 2014

Klose sasa ngoma droo na Ronaldo,Ujerumani wanusurika kwa Ghana.

Lionel Messi amefunga Bao katika Dakika ya 91 na kuipa Argentina ushindi wa Bao 1-0 kwenye Mechi ya Kundi F la Fainali za Kombe la Dunia iliyochezwa Estadio Mineirão Mjini Belo Horizonte Nchini Brazil.
Ira, chini ya Kocha Carlos Quieroz ambae aliwahi kuwa Manchester United, walisimama kidete kuisimamisha Argentina na walipata nafasi ya wao kufunga wakati kichwa cha Ashkan Dejagah kilipookolewa na Kipa Sergio Romero.
Baadaye, Mechi nyingine ya Kundi F itachezwa kati ya Nigeria na Bosnia.MESSI_IN_ARGENTINA
Argentina wamebakisha Mechi moja na watacheza na Nigeria hapo Jumatano Juni 25.
Goli la Miroslav Klose dakika ya 71 limeinusuru Ujerumani kulala mbele ya Ghana, baada ya kulazimisha sare ya 2-2 muda mfupi uliopita  katika mchezo wa Kundi G Kombe la Dunia mjini Fortaleza, Brazil.
Klose sasa amefikisha jumla ya mabao 15 katika Kombe la Dunia na kumfikia mfungaji bora wa kihistoria wa michuano hiyo, Mbrazil Ronaldo de Lima, ambaye tayari ameshastaafu soka.
Ujerumani ilianza kupata goli dakika ya 51 kupitia kwa  Mario Gotze alianza kuifungia , lakini Andre Ayew akaisawazishia Ghana dakika ya 54 kabla ya Asamoah Gyan kuifungia Black Stars bao la pili dakika ya 63.
Ghana wakashindwa kuulinda ushindi wao na Klose akaisawazishia Ujerumani dakika ya 71.
WACHEZAJI WALIOFUNGA MABAO MENGI KOMBE LA DUNIA
   Mchezaji/Nchi     Mabao   
Ronaldo-Brazil 15
Miroslav Klose-Ujerumani 15
Gerd Muller-Ujerumani 14 
 Just Fontaine-Ufaransa 13
 Pele-Brazil 12 
 Sandor Kocsis-Hungary 11 
 Jurgen Klinsmann-Ujerumani 11 
 Helmut Rahn-Ujerumani 10 
 Gary Lineker-uingereza 10 
 Gabriel Batistuta-Argentina 10 

0 comments:

Post a Comment