Tchakala kocha mpya Togo
Waziri wa michezo nchini Togo amethibitisha rasmi uteuzi wa Tchanilé Tchakala kuwa kocha mpya wa timu hiyo baada ya mkataba wa aliyekuwa kocha wa Togo mfaransa Didier Six kutoongezwa mwezi januari..Tchakala alikuwa msaidizi wa Six na pia aliwahi kuwa katika benchi la ufundi mwaka 2013 katika mashindno ya AFCON .
Tchakala ni kaka wa Tchanilé Bana, ambaye aliifundisha Togo kati ya mwaka 2000 na 2002 ambaye alituhumiwa kuiongoza Togo kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Bahrain September 2010. Kocha huyo ataanza kibarua cha kuiongoza Togo kufuzu mashindano ya mataifa ya Afrika kule nchini Morocco.
Amepewa mkataba wa miezi sita na utaongezwa iwapo ataonsha kazi nzuri,kwa mujibu wa waziri wa michezo.
0 comments:
Post a Comment