Wednesday, 25 June 2014

Breaking news;Barcelona kumsajili kipa wa Chile.

Klabu ya Barcelona ya Hispania imesema kuwa itamsajili golkipa wa timu ya taifa ya Chile  Claudio Bravo na itampatia mkataba wa miaka minne baada ya makubaliano kwenda vema na klabu yake ya  Real Sociedad.
Barcelona haijatoa maelezo ya kutosha kuhusu dili hilo.
Barcelona imesema kuwa  Bravo atasaidiana na kipa wao mpya Marc-Andre ter Stegen baada ya  Victor Valdes kumaliza mkataba wake.
Bravo mwenye miaka  31 ndiye nahodha wa Chile ambayo kwa sasa yuko nchini Brazil katika fainali za kombe la dunia na Chile itacheza na Brazil katika hatua ya mtoano.
Ikumbukwe kuwa Bravo  ameitumikia Sociedad misimu minane baada ya kuanza soka akiwa na klabu ya kule nchini kwao,Colo-Colo.
Akifanikiwa kujiunga na Baka  atakutana na Mchile mwenzake Alexis Sanchez

0 comments:

Post a Comment