Saturday, 21 June 2014

Uingereza nje,pata ratiba ya leo kombe la dunia

Bao la Dakika ya 44 Bryan Ruiz, anaechezea Fulham, limewapa ushindi wa Bao 1-0 Costa Rica walipocheza na Italia huko Arena Pernambuco, Jijini Fortaleza Nchini Brazil kwenye Mechi ya Kundi D la Fainali za Kombe la Dunia.
Mbali ya Costa Rica kushinda, Matokeo hayo sasa yamethibitisha rasmi Uingereza  wako nje ya Fainali hizi na sasa watakamilisha Ratiba tu kwa kucheza na Costa Rica Mechi ya mwisho hapo Jumanne Juni 24.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Uingereza kutolewa hatua za makundi baada ya miaka 56 iliyopita.
Matokeo mengine jana  Ufaransa  imejiweka nafasi nzuri mno ya kutinga Raundi ya Pili ya Mtoano ya Fainali za Kombe la Dunia baada kuitandika Switzerland mabao 5-2 katika Mechi yao ya Kundi E iliyochezwa huko Arena Fonte Nova huko Jijini Salvador.
Katika Mechi nyingine ya Kundi E hiyo Jana, Ecuador iliwafunga Honduras mabao 2-1 na kujikita nafasi ya Pili nyuma ya Ufaransa.
Hii leo Kevin-Prince Boateng na Jerome Boateng ambao ni ndugu  watakutana uso kwa uso kwenye Mechi ya Kundi G la Fainali za Kombe la Dunia huko Estadio Castelão Mjini Fortaleza, Brazil.
Siku hiyo, Ghana itaivaa Ujerumani kwenye Mechi zao za Pili za Kundi G huku Ghana wakiwania ushindi baada ya kufungwa Mechi yao ya kwanza na Marekani mabao 2-1 na Ujerumani ikitaka kuendeleza ushindi baada ya kuichapa Ureno mabao 4-0.
Kevin-Prince Boateng, anaechezea Ghana, ameeleza pambano hilo litakuwa la ‘kufa na kupona’ wakati atakapokabiliana na Ndugu yake Jerome Boateng anaechezea Ujerumani.
Mwaka 2010, huko Afrika Kusini, kwenye Fainali za Kombe la Dunia, Kevin-Prince na Jerome, walivaana wakati Nchi zao zilipokutana na kuweka Historia ya kuwa Ndugu wa kwanza kabisa kuchezea Timu pinzani.
JUMAMOSI, JUNI 21, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Argentina v Iran
F
Estadio Mineirão
2200
Germany v Ghana
G
Estadio Castelão
0100
Nigeria v Bosnia-Herzegovina
F
Arena Pantanal

0 comments:

Post a Comment