Tuesday, 3 June 2014

Ulingo wa mieleka;Hatimaye wale wababe wa Shield wajichanganya,Batista naye awakacha wenzake pata uhondo hapa

Baada ya kukaa zaidi ya miaka miwili kama kikundi, hatimaye kikundi cha Shield  kimevunjika rasmi jana baada ya mwanamieleka wao moja kujitoa,anaitwa Seth Rollins.
Kikundi hicho kilivunjika baada ya Seth Rollins Kuanza kuwapiga wenzake akina Dean Ambrose, Roman Reigns bila sababu yoyote huku  wakisubiri kikundi cha Evolution ambacho pia kilivunjika mapema jana baada ya Batista kujitoa  ili wapande jukwaani.
Mpaka sasa haijaelezwa wazi kwanini Seth Rollins alianza kuwasaliti lakini baada ya kuhitimisha shambulizi hilo alienda moja kwa moja mikononi mwa Triple H ambaye ndiye kiongozi wa Kikundi cha Shield na ni wazi kuwa amaejiunga na Evolution.
Sports4lifetz inaelewa wazi kuwa Kwa takriban miezi kadhaa sasa mchezo wa mieleka umetawaliwa na vikundi hivi viwili vya Shield pamoja na Evolution ambapo juni 1 Shield waliwapiga Evolution kwa mara nyingine katika michezo ya Payback na Exterme Rules.
Ikumbukwe kuwa usiku wa jumapili wanamieleka mbalimbali walishuka dimbani na matokeo ni kwamba  John Cena alionesha jinsi gani alivyokuwa na uwezo baada ya kumpiga Bray Wyatt kwenye mchezo ulioitwa Last Man Standing .
Sheamus ambaye ni bingwa wa Marekani alimpiga  Cesaro na kutwaa ubingwa wa United States .
Bad News Barrett alibeba ubingwa wa mabara baada ya kumpiga bingwa wa zamani wa uzito wa juu Rob Van Dam.
Ryback na Curtis Axel walishinda dhidi ya  Cody Rhodes na Goldust
Rusev alimpiga Big E.
Kwa mara nyingine ubingwa wa akina dada maarufu kama Divas umebebwa tena na Paige  baada ya kumpiga Alicia Fox.
Shield walijiunga rasmi na michezo ya mieleka mwaka 2012 mpaka sasa wakiwa na muungano wa wanamieleka watatu lakini baada ya tukio la jana sasa wamebaki wawili tu.
Evolution kikundi chao kiliundwa na Triple H,Randy Orton pamoja na Batista aliyejitoa lakini sasa Sethi Rolins atakuwa mwanachama wao  mpya akichukua nafasi ya mnyama Batista.
Sports4lifetz itaendleea kufuatilia mwenendo wa vikundi hivyo.


0 comments:

Post a Comment