Wednesday, 4 June 2014

Wachezaji wenye thamani duniani,Suares,Ronaldo na Messi balaaaa

Nyota wa kimataifa wa Uruguay, Luis Suarez ameshika nafasi ya tatu katika orodha ya wachezaji soka wenye thamani zaidi duniani iliyochapishwa leo, akikadiriwa kuwa na thamani ya paundi milioni 79.
Lionel Messi ndio anayeongoza orodha hiyo akikadiriwa kuwa na thamani ya paundi milioni 161.5 akifuatiwa na Cristiano Ronaldo mwenye thamani ya paundi milioni 85.2 kwa mujibu wa jarida la Think Tank lenye maskani yake nchini Switzerland.
Orodha hiyo imezingatia bei ya sasa ya kila mchezaji katika soko la usajili kwa kuzingatia mkataba wake uliobakia, nafasi , kiwango, na uzoefu wa kimataifa.
Nafasi ya nne katika orodha hiyo imeshikiliwa na nyota wa kimataifa wa Ubelgiji na Chelsea Eden Hazard anayekadiriwa kuwa na thamani ya paundi milioni 61.2 ambapo Chelsea walilipa nusu ya pesa hiyo ili kupata saini yake miaka miwili iliyopita.
Nafasi ya tano inashikiliwa na Neymar mwenye thamani ya paundi milioni 50.6, akifuatiwa na Paul Pogba wa Juventus paundi milioni 48.9, Gareth Bale wa Real Madrid paundi milioni 47.1 kiwango ambacho ni cha chini ikilingashwa na kile alichonunuliwa mwaka jana.
Wengine Mesut Ozil wa Arsenal paundi milioni 39.7 akifuatiwa na Edinson Cavani wa PSG paundi milioni 38.7 na kumi bora inafungwa na Mario Gotze wa Bayern Munich paundi milioni 37.9.

0 comments:

Post a Comment