Kukosekana kwa Diego Costa si kigezo cha sisi kukosa ubingwa-Del Bosgue
Kocha wa timu ya taifa ya Hispania,
Vicente Del Bosque amekanusha kuwa nafasi ya kikosi chake kutetea taji la Kombe
la Dunia itaingia dosari kama Diego Costa hatakuwa fiti.
Kocha huyo aliamua kubahatisha kwa
kumjumuisha nyota huyo wa Atletico Madrid katika kikosi chake cha mwisho pamoja
na mshambuliaji mwenye umri wa miaka 25 kuwa majeruhi aliyopata katika kipindi
cha mwisho cha msimu.
Del Bosque anetegemea Costa ambaye
alifunga mabao 36 katika mashindano yote msimu uliopita akiwa na klabu yake,
kiongozi katika safu ya ushambuliaji mbele ya Fernando Torres na David Villa.
Ingawa anapona taratibu nyota
huyo mzaliwa wa Brazil ameanza kufanya mazoezi kama kawaida na kikosi cha nchi
hiyo Jumatatu kuelekea katika mchezo wao wa mwisho wa kirafiki kabla ya Kombe
la Dunia.
Akihojiwa kuhusiana na hilo Del
Bosque amesema watu wamekuwa wakimuuliza swali hilo wakati wa michuano ya Ulaya
mwaka 2012 ambayo walikuwa mabingwa huku wengine wakidai alitumia mfumo
usiokuwa na mshambuliaji yaani 4-6-0.
Del Bosque amesema ni kweli
angependa Costa awemo katika kikosi chake cha mwisho lakini kama hatakuwa fiti
kwa asilimia 100 itabidi afanye maamuzi kabla ya kutangaza kikosi cha mwisho,
hata hivyo bado anaamini anatakuwa fiti kwa ajili ya michuano hiyo.
0 comments:
Post a Comment