Monday, 23 June 2014

Waliofunga mabao mengi mpaka sasa kombe la dunia 2014

Wakati fainali za kombe la dunia zikiwa zinamaliza mechi zake za mwisho hii leo kwa upande wa makundi,baadhi ya wachezaji wameshaingia kwenye list ya wanaowania tuzo za mfungaji bora kwa upande wa mabao.
Hawa ni baadhi tu ya wale ambao wameonekana kufunga mabao mengi kwa sasa mwaka 2014 kule Brazil.
Thomas Muller (Ujerumani ), Robin Van Persie, Robben (Uholanzi), Karim Benzema (Ufaransa) pamoja na E Valencia (wa Ecuador) wana mabao 3 kila moja.
Neymar da Silva (Brazil), Lionel Messi (Argentina), Tim Cahill (Australia), Mario Mandzukic (Croatia), LUIS Suarez (Uruguay), Gervinho (Ivory Coast), Rodriguez (Colombia), Dempsey (USA), A Ayew (Ghana). wana mabao 2 kila mmoja.
Kabla ya michezo ya leo kuna baadhi ya wachezaji wasipofunga ndio itakuwa mwisho wao kutokana na timu zao kufungashwa virago mfano ni Cahil wa Australia.
Lakini iwapo Neymar,Mario Mandzukic,Robben au Van Persie wakifunga bao leo watajiongezea  kwenye hazina yao.
Leo JUMATATU, JUNI 23, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Australia v Spain
B
Arena da Baixada
1900
Netherlands v Chile
B
Arena Corinthians
2300
Croatia v Mexico
A
Arena Pernambuco
2300
Cameroon v Brazil
A
Nacional

0 comments:

Post a Comment