Monday, 23 June 2014

Van Gaal akerwa na wanahabari kombe la dunia

Luis Van Gaal
Kocha wa Uholanzi, Luis Van Gaal, amewashambulia wanahabari wa taifa lake wanaomulika Kombe la Dunia baada ya maelezo kuhusu kikao cha mazoezi kilichofungwa kufichuka kabla ya mechi yao dhidi ya Chile.
Van Gaal alisema kufichua mipango yao ambayo ilitibua kuwa mkongwe Dirk Kuyt angelichukua nafasi ya Robin Van Persie haitasaidi chochote.
“Sipendelei mambo kama haya yakitolewa hadharani na wanahabari wa Uholanzi au wa kutoka popote kwani haisaidii. Itachangia tu kutuletea matatizo.
“Sielewi ni kwa nini jambo hili lilifanyika kwani ni fikira yangu kuwa tunafaa kuwa pamoja hapa lakini ni bayana hilo haliwezi fanyika,”kocha  huyo atakayechukua hatamu za uongozi za Manchester United baada ya shindano hili alikemea maripota.
Ingawa vikao vya mazoezi huruhusu wanahabari, sehemu zingine hufungwa ili vikosi vinoe mipango na mbinu zao kwa siri.
Van Gaal alikataa kujadiliana kuhusu mabadiliko ili Chile wasinufaike kabla ya kivumbi chao cha mwisho Kundi B Jumatatu.
Timu zote zimefuzu lakini mshindi au Uholanzi wakidhibiti Chile sare ataibuka kama kiongozi wa kundi hilo na kuepuka wenyeji Brazil kwenye Raundi ya 16 bora ambayo ni mwondoano.

0 comments:

Post a Comment