Yobo kuweka rekodi mbele ya Ufaransa.
Nahodha wa Nigeria, Joseph Yobo, anatarajia kuwa mchezaji wa kwanza wa Nigeria kucheza michezo 100 katika timu ya taifa ya nchi hiyo wakati mabingwa hao wa Afrika watakapocheza na Ufaransa hapo baadaye katika kombe la dunia..Yobo alianza kucheza mashindano ya kimataifa ya kombe la dunia kwa upande wa vijana chini ya umri wa miaka 20 (Fifa Under-20 World ) mwaka 1999.
Inapendeza kusikia kuwa Iker Casillas wa Hispania, Diego Forlan wa Uruguay, Rafael Marquez wa Mexico, Tim Howard wa USA, Julio Cesar wa Brazil, Xavi wa Spain, Stipe Pletikosa wa Croatia na Mark Bresciano wa Australia ni baadhi ya wachezaji waliowakilisha nchi zao mwaka 1999 kama ilivyo kwa Yobo.
Hivyo basi, Yobo atapata bahati hiyo katika mashindano makubwa iwapo akipangwa mchezo wa leo na kuungana na akina Pletikosa, Marquez, Xavi, Casillas, Forlan na Howard kama nyota wa 1999 ili kufikisha mchezo wake wa 100 .
Yobo mwenye miaka 33 ameisaidia Nigeria kuwa mabingwa wa Afrika pia timu imeingia 16 bora ya kombe la dunia na alianza kucheza timu ya wakubwa mwaka 2001.
Akizungumzia hilo,Yobo amesema anapata faraja baada ya kubeba ubingwa wa Afrika na hatimaye kucheza kombe la dunia na kuongeza kuwa lazima waitoe Ufaransa na kutinga robo fainali.
JOSEPH YOBO | |||
---|---|---|---|
Jina kamili | Joseph Phillip Yobo | ||
Kuzaliwa | 6 September 1980 | ||
Alopozaliwa | Kono, Nigeria | ||
Urefu | 1.88 m (6 ft 2 in) | ||
Nafasi uwanjani | Mlinzi | ||
0 comments:
Post a Comment