Klose na Rekodi ya mabao kwa timu za Afrika,leo ataweka rekodi mbele ya Algeria? Ronaldo alifanya hivyo.
Baada ya Mchezaji Miroslav Klose wa Ujerumani kufanikiwa kusawazisha rekodi iliyokuwa inashikiliwa na nyota wa zamani wa Brazil Ronaldo de Lima ya kufunga mabao 15 katika fainali za kombe la dunia,leo wengi wanasubiri iwapo atavunja rekodi hiyo.Mshambuliaji huyo mwenye miaka 36 ambaye mwaka huu anacheza fainali zake za nne alifunga bao lake la 15 la mashindano ya kombe la dunia katika dakika ya 71 na ni bao lake la 69 katika mashindano ya kimataifa,Ujerumani ilipocheza na Ghana.
Klose mfungaji bora wa kombe la dunia mwaka 2006 akiwa na mabao 5 alimaliza akiwa wa pili mwaka 2002 akifunga mabao 5 pia na kule Afrika ya kusini mwaka 2010.
Akifunga bao katika mchezo wao dhidi ya Algeria usiku wa leo atakuwa amefikisha mabao 16 na kumpiku Ronaldo.
Sports4lifetz imebaaini kuwa Ronaldo aliweka rekodi ya kufunga mabao hayo 15 wakati Brazil ikicheza na Ghana katika fainali za kombe la dunia mwaka 2006 pia Klose amefunga bao lake la 15 mchezo dhidi ya Waafrika yaani Ghana.
Ni wazi kuwa Ronaldo na Klose wameweka rekodi zao mbele ya timu za Afrika ambayo ni Ghana.
Je leo Klose ataweka rekodi mbele ya Algeria ambayo inatoka bara la Afrika?????? swali litapata jibu leo usiku.
Kwa upande wake Thomas Muller akifanikiwa kufunga bao leo atakuwa amefikisha mabao kumi toka aanze kucheza kombe la dunia na litakuwa bao lake la 5 kwa mwaka huu na ataingia kwenye kumi bora.
WACHEZAJI WALIOFUNGA MABAO MENGI KOMBE LA DUNIA
Mchezaji/Nchi | Mabao |
Ronaldo-Brazil | 15 |
Miroslav Klose-Ujerumani | 15 |
Gerd Muller-Ujerumani | 14 |
Just Fontaine-Ufaransa | 13 |
Pele-Brazil | 12 |
Sandor Kocsis-Hungary | 11 |
Jurgen Klinsmann-Ujerumani | 11 |
Helmut Rahn-Ujerumani | 10 |
Gary Lineker-uingereza | 10 |
Gabriel Batistuta-Argentina | 10 |
0 comments:
Post a Comment