Apumzike kwa amani,Toure azikwa Ijumaa
![]() |
Ibrahim Toure,enzi za uhai wake |
Mamia ya mashabiki walivaa mavazi meupe ili kutoa heshima zao za mwisho kwa mshambuliaji huyo mwenye miaka 29.
![]() | |
Familia ya Toure |
Toure hakuwa maarufu sana kutokana na kutoitwa timu ya taifa lakini msiba wake ulishtua watu wengi baada ya kaka zake kuwepo kwenye mashindano ya kombe la dunia 2014 Brazil wakiiwakilisaha Ivory Coast.
Kama ilivyo kwa kaka yake,Toure alianza soka katika akademi ya Asec Mimosas ya mjini Abidjan. Aliwahi kuicheza Lebanese ya Al Safa, Metallurg Donestk nchini Ukraine, klabu ya Nice ya Ufarana na Misr El Maqasa ya Misri.
0 comments:
Post a Comment