Sunday, 6 July 2014

Uholanzi yatinga nusu fainali kucheza na Argentina,Angel Di Maria nje kombe la dunia.

Timu ya taifa ya Uholanzi imeingia hatua ya nusu fainali baada ya kushinda kwa mikwaju ya pelnati   4-3 dhidi ya  Costa Rica,baada ya dakika 120 matokeo ikiwa ni suluhu.
Golkipa wa Newcastle Tim Krul  aliingizwa dakika za mwisho  kabla ya filimbi ya mwisho na kocha wake  Louis van Gaal - mabadiliko yaliyoonesha matokeo mazuri kwa Uholanzi.
Costa Rica iliwadhibiti sana Uholanzi katika nafasi ya Ulinzi huku kipa Keylor Navas aking'ara golini.
Wesley Sneijder alikosasakosa mabao baada ya shuti zake mbili kugonga mwamba wa pembeni na wa juu.
Kipa aliyetoka benchi  Tim Krul, aliokoa pelnati ya nahodha wa Costarica  Bryan Ruiz na pelnati ya Michael Umana na timu kushinda  4-3.

Wakati hayo yakiendelea  mchezaji wa Argentina Angel Di Maria atakosa mechi za kombe la dunia kwa timu yake baada ya kuumia msuli wa nyama ya pajani wakati Argentina ikiibamiza Ubelgiji bao 1-0 katika mchezo wa kwanza mapema leo.
Brazil itapambana na Ujerumani  mechi ya nusu fainali huku  Neymar akikosekana ilhali Uholanzi itacheza na Argentina.
NUSU FAINALI
JUMANNE, JULAI 8, 2014

SAA MECHI KUNDI UWANJA
2300  Ujerumani v Brazil [61] NUSU FAINALI Estadio Mineirão, Belo Horizonte
JUMATANO, JULAI 9, 2014
SAA MECHI KUNDI UWANJA
2300 Argentina v Uholanzi  [62] NUSU FAINALI Arena Corinthians, Sao Paulo
MSHINDI WA TATU
JUMAMOSI, JULAI 12, 2014

SAA MECHI KUNDI UWANJA
2300 Aliyefungwa 61 v Aliyefungwa 62 MSHINDI WA 3 Nacional, Brasilia
FAINALI
JUMAPILI, JULAI 13, 2014

SAA MECHI KUNDI UWANJA
2200 Mshindi Mechi 61 v Mshindi Mechi 62 FAINALI Estadio do Maracanã, Rio de Janeiro


0 comments:

Post a Comment