Beki wa Uholanzi hatihati kucheza kesho.
Beki wa Uholanzi, Ron Vlaar, anasumbuliwa na jeraha la goti ambalo linaweza kumwondoa kwenye nusu fainali ya Kombe la Dunia Jumatano dhidi ya Argentina.Maafisa wa kikosi hicho walitangaza kuwa Vlaar alikosa mazoezi ya Jumapili baada ya kupata jeraha hilo kwenye ushindi wao wa robo fainali dhidi ya Costa Rica kupitia mikwaju ya penalti.
Vlaar ameshamiri kwenye kikosi chake kilicho tamba kwenye mechi za makundi kwa kishindo walipocharaza mabingwa wa dunia Uhispania 5-1 kisha kuwachakaza Mexico na Costa Rica.
Mkataba wa beki huyo, 29, na klabu Feyenoord ya Uholanzi imekamilika na kocha wake wa taifa, Luis Van Gaal, anasemekana atambeba hadi Manchester United kuelekea Uingereza ambapo atafundisha kwa msimu ujao.
0 comments:
Post a Comment