Tuesday, 8 July 2014

Nusu fainali kombe la dunia,Scolari"Nipo vizuri" ila Wajerumani walia na mwamzi,

Ni kama fainali ya mwaka 2002.Mchezo wa Nusu fainali ya kwanza ya kombe la dunia nchini Brazil 2014 utapigwa leo(jumanne Julai 8),wenyeji  Brazil watacheza na Ujerumani,mchezo huo utachezeshwa na mwamuzi Marco Rodriguez.
Nyota wa Ujerumani, Bastian Schweinsteiger amesihi mwamuzi Marco Rodriguez adhibiti na awe makini dhidi ya mchezo wa dhuluma kutoka wenyeji.
Mwamuzi huyo alisimamia mechi ya Uruguay na Italia ambayo Luis Suarez alishambulia mpinzani Giorgio Cheillini kwa meno ingawa hakuona kisa hicho kilichosababisha mshambuliaji huyo kupigwa marufuku miezi minne.
Schweinsteiger hataki marudio ya mchezo mbaya ulioonyeshwa na Brazil kwenye ushindi wao wa 2-1 dhidi ya Colombia kwenye robo fainali ambapo vijana wa La Selacao walizuia wapinzani wao kutandaza mpira wao kwa kuwaandama vikali kutoka mwanzo hadi mwisho.
Leo nahodha Tiago Silva na Neymar watakosa mchezo huku Neymar ameifungia Brazil mabao 4 kati ya 8 waliyofunga kwenye Fainali hizi lakini hatashiriki Mechi zilizobaki baada ya kuvunjwa Mfupa mdogo wa Mgongoni kwenye Mechi iliyopita ya Robo Fainali ambayo waliitoa Colombia Bao 2-1. lakini Silva anatumikia adhabu ya kadi mbili za njano
“Sina shida na mchezo mgumu lakini kuna makosa yaliyopita kipimo. Kikosi cha sasa cha Brazil si wachawi wa kale. Mchezo wao umebadilika.
“Kukabiliana vikali na wapinzani wao imekuwa ndio mtindo wao mpya, ni jambo tunalofaa kutahadhari na pia mwamuzi,” Schweinsteiger alisema.
“Brazil wana wachezaji wenye uwezo mkubwa kiufundi lakini wanahujumu wapinzani wao na ni lazima mwamuzi awe mwangalifu,” Kocha wake, Joachim Loew, aliongeza.
Naye Kocha wa Brazil Luis Scolari amesema Kikosi chake kitamudu bila nyota wao aliyeumia Neymar.
Neymar ameifungia Brazil mabao 4 kati ya 8 waliyofunga kwenye Fainali hizi lakini hatashiriki Mechi zilizobaki baada ya kuvunjwa Mfupa mdogo wa Mgongoni kwenye Mechi iliyopita ya Robo Fainali ambayo waliitoa Colombia Bao 2-1.
Scolari amedai Kikosi chake kipo vizurii na wanatilia mkazo Mechi hii ya Leo.

0 comments:

Post a Comment