Wednesday, 2 July 2014

Bora Suarez aliyeng'ata kuliko Matuidi aliyefanya faulu mbaya-Maradona.

Nyota wa zamani wa Argentina , Diego Maradona, amesema kuwa ule ni uhalifu kwa mchezaji wa Ufaransa Blaise Matuidi kumchezea vibaya kiungo wa Nigeria Ogenyi Onazi katika mchezo wa mtoano hatua ya 16 kombe la dunia kati ya Ufaransa na Nigeria. Maradona, ambaye ni mchambuzi katika runinga yaVenezuela, Telesur TV, amemkashifu mwamuzi kutoka Marekani , Mark Geiger kwa kile alichodai kuwa hakuona tukio hilo kama uhalifu wa hali ya juu dhidi ya Matuidi.
Maradona amesema kuwa mfaransa huyo alimfanyia makosa makubwa sana Onazi na ni hatari kuliko ya  Luis Suarez aliyemng'ata meno mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini.
"Haiwezekani mwamuzi kutokuchukulia tukio lile kama uhalifu. Ilikuwa mbaya sana kuliko aliyoyafanya  Suarez dhidi ya  Chiellini," alisema Maradona
Matuidi alitenda tukio hilo ambapo Ufaransa ilishinda mabao 2-0 na baada ya mchezo kumalizika alikwenda kuomba msamaha ndani ya chumba cha kubadilishia nguo cha Nigeria.

1 comments:

Unknown said...

Maradona kasema ukweli,Msamaha wa nini wakati aliishatuumiza na ndichio chanzo cha kuidhoofisha timu yetu???Nawashangaa FIFA kwa nini wanakataa kutumia ushahidi wa video kutoa haki wakati wanaweza kumuadhibu mtu kwa kutumia ushahidi wa video???Wapuuzi sana

3 July 2014 at 14:32

Post a Comment