Brazil na Ujerumani kuchezeshwa na mwamuzi aliyechezesha Uruguay na Italia
Shirikisho la soka dunianai FIFA imetangaza mwamuzi wa Mechi ya Nusu Fainali ya Kombe la Dunia kati ya Brazil na Ujerumani.
Mwamuzi huyo ni yule aliyechezesha mchezo
ambao sasa umeshika vichwa vya watu wengi Duniani kati ya Italia na Uruguay katika kombe la
Dunia huko Brazil ambapo mchezaji wa Uruguay, Luis Suarez, alimng’ata
Meno Beki wa Italia Giorgio Chiellini bila mwaamuzi huyo kuona tukio hilo na
kutochukua hatua yeyote hata baada ya Chiellini kumkimbilia na kuvua
Jezi kuonyesha alama za Meno.
Mwamuzi huyo kutoka Mexico ni Marco
Rodríguez, mwenye Miaka 40 atasimama katikati ya uwanja hiyo kesho
Hii ni mara ya 3 kwa mwamuzi huyo kuchezesha Fainali za Kombe la Dunia,Mbali ya Mechi ya Uruguay na Italy, pia amechezesha Mechi nyingine huko Brazil ni
ile ya Ubelgiji v. Algeria.
0 comments:
Post a Comment