Kocha wa Algeria ajiuzulu japo rais Bouteflika alimwambia aendelee na kazi.
Kocha wa Algeria Vahid Halilhodzic amethibitisha kuacha kuifundisha timu ya taifa ya nchi hiyo japo ameombwa na rais wa nchi ili aendelee kuinoa timu hiyo baada ya kuingia hatua ya 16 bora kombe la dunia kule Brazil.Raia huyo wa Bosnian amethibitisha kuondoka kwake kwenye mtandao wa shirikisho la soka la Algeria, Algeria Football Federation yaani (www.faf.dz).
Halilhodzic aliombwa na rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika ili aendelee na kazi ya ukocha kwenye kikosi hicho baada ya kupokelewa kwa ushujaa mjini Algiers baada ya kufungwa na Ujerumani katika 16 bora.
Algeria ilifungwa mabao 2-1 katika muda wa nyongeza jumatatu iliyopia katika mji wa Porto Alegre.
Kocha huyo mwenye miaka 61 anatarajia kuwa kocha mpya wa klabu ya Trabzonspor ya Uturuki wiki ijayo.
Algeria wamekwisha anza maongezi na mfaransa Christian Gourcuff ili awe mrithi wa Halilhodzic amabaye alishasema mwanzoni kuwa hataongeza mkataba baada ya kombe la dunia.
Halilhodzic,mshambuliaji wa zamani wa Yugoslavia ameipa Algeria sifa ya kuingia 16 kwa mara ya kwanza kombe la dunia.
0 comments:
Post a Comment