Wednesday, 9 July 2014

David Luiz aomba msamaha baada ya kipigo cha 7-1

Beki na nahodha msaidizi wa timu ya taifa ya Brazil, David Luiz , ameomba radhi mashabiki wa soka wa nchi hiyo kufuatia kipigo cha mabao 7-1 walichokipokea kutoka kwa Ujerumani jana  usiku mjini Belo Horizonte.
Ndoto za Brazil kubeba kombe kama wenyeji zilitoweka  baada ya Ujerumani kuongoza mabao 5-0 katika kipindi cha kwanza.
Shabiki akitokwa na machozi
Luiz, ambaye alichukua jukumu la kukiongoza kikosi cha Brazil kufuatia nahodha Thiago Silva, kutumikia adhabu ya kuonyeshwa kadi mbili za njano, amesema mpaka sasa hawajui nini kilichosababisha kupokea kipigo hicho ambacho kinaiingiza nchi hiyo katika rekodi mpya kwenye medani ya soka duniani.
Amesema wanatambua mashabiki wa soka nchini humo, wameumizwa  na kichapo hicho, lakini akasisitiza hawana budi kusamehewa na kuendeleza umoja waliokuwa nao kama walivyoanza fainali za kombe la dunia za mwaka huu June 12.
''Katika maisha yangu,nimejifunza kuwa m
Mashabiki hawaamini kinachoendelea Brazil v Ujerumani
tu wa muda wote.Sitaona aibu kwa chochote kile.Siku moja nitwapa mashabiki furaha'' Alisema Luiz.
Kwa upande wa mlinda mlango wa Brazil, Julio Cesar amesema soka lina maajabu yake na usiku wa kuamkia hii leo, maajabu ya hatari yaliwageukia wao kama wenyeji, hivyo hawana budi kukubaliana na hili hiyo.
Timu ya taifa ya Brazil imekubali kufungwa mabao 7-1 na kuwa timu ya kwanza duniani kufungwa idadi hiyo ya mabao katika mchezo wa hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la dunia.

0 comments:

Post a Comment