Wednesday, 9 July 2014

Klose ampiku Ronaldo,Muller aingia kwenye kumi bora....wengine hawa hapa.

Mshambuliaji wa Ujerumani Miroslav Klose ameweka rekodi ya kuwa mfungaji mabao mengi zadi katika historia ya kombe la dunia.
Klose alifunga bao la pili Ujerumani ilipoilaza Brazil mabao 7-1 katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la dunia huko,Brazil.
Klose  amefunga sasa jumla ya mabao 16 baada ya kushiriki michuano nne za kombe la dunia.
Mshambulizi huyo alikuwa ana mabao sawa na nyota  wa zamani wa rekodi hiyo mbrazil Ronaldo alipoifungia Ujerumani bao la pili la kusawazishia dhidi ya Ghana katika mechi za mchujo awali katika kipute hicho.

Klose amefunga mabao 16
Wakati huohuo mshambulizi huyo alivunjilia mbali rekodi ya mfungaji mabao mengi zaidi ya kimataifa kwa mjerumani alipoifungia timu yake bao la 68 Ujerumani ilipokuwa ikishiriki mechi ya kirafiki dhidi ya Armenia.
Rekodi ya awali ya Ujerumani ilikuwa inashikiliwa na Gerd Mueller
Naye Thomas Muller amefikisha mabao kumi tokea aanze kucheza kombe la dunia baada ya jana kufunga bao lake la 5 la mashindano ya mwaka huu.
Kufuatia Ushindi huo Ujerumani imefuzu kwa fainali yake ya kwanza katika kipindi cha miaka kumi na miwili iliyopita.
Ronaldo De lima
Sport4lifetz inakuletea kumi bora ya wachezaji waliofunga mabao mengi zaidi,Anayemfuata kwa karibu Ronaldo ana mabao  14 ambaye ni mjerumani  ambaye hachezi soka kwa sasa Gerd Muller,.

   Mchezaji/Nchi     Mabao   
Miroslav Klose-Ujerumani 16
Ronaldo-Brazil 15
Gerd Muller-Ujerumani 14 
 Just Fontaine-Ufaransa 13
 Pele-Brazil 12 
 Sandor Kocsis-Hungary 11 
 Jurgen Klinsmann-Ujerumani 11 
 Helmut Rahn-na Thomas Muller-Ujerumani 10 
 Gary Lineker-uingereza 10 
 Gabriel Batistuta-Argentina 10 
Muller aliyecheza soka miaka ya 1970 na  1974 na kufunga bao kwa wastani wa 1.08 kwa mchezo moja wa kombe la dunia.

Nyota wa zamani wa Ufaransa  aliyecheza soka miaka ya 1958 Just Fontaine - amefunga mabao  13 .
Akiwa na mabao 12 katika mashindano nne ya kombe la dunia  kuanzia  1958 na 1970, gwiji wa Brazil  Pele ni nyota kwenye nchi yake akiwa na mabao hayo na kubeba kombe mara 3

Wachezaji wawili wamefunga mabao  11 kila moja , gwiji wa Hungary  Sandor Kocsis na Mjerumani   Jurgen Klinsmann.
Kumi bora inafungwa na Mjerumani  , Helmut Rahn, mwaka wa 1954 na 1958, mshambuliaji wa
Pele.
zamani wa Uingereza  Gary Lineker pamoja na Muarjentina, Gabriel Batistuta.
Taarifa hizi ni kwa mujibu wa Sports4lifetz kushirikiana na Goal.com

0 comments:

Post a Comment