Wednesday, 2 July 2014

Kozi ya ukocha ngazi ya kati mkoani Tabora imeanza,wadau waombwa kujitokeza

Shija Simon,kulia-Mshiriki
Kozi ya makocha wa ngazi ya pili (Intermediate) inayosimamiwa na Chama cha makocha mkoa wa Tabora imeanza jana na kuendelea kwa siku yake ya pili.

Kozi hiyo ilianza Julai 1 mwaka huu kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, uliopo mkoani Tabora Kozi hiyo iko chini ya Mkufunzi Meja Kigange, kutoka Dar es Salam ambapo makocha mbalimbali pamoja na wachezaji wa zamani wamejitokeza kushiriki.
Katibu wa chama cha makocha Tabora bwana Andrew Zoma jana alisema kozi hiyo imeanza kwa kusuasua ambapo washiriki 20 wamejitokeza kwa siku ya jana na kuomba wadau mbalimbali wenye sifa kujitokeza kwa wingi ili kuitumia nafasi hiyo adimu.
Zoma ameongeza kuwa kwa yeyeote yule aliyepitia ngazi ya kwanza ana fursa ya kushiriki na pia wameongeza muda wa siku mbili ili watu wenye sifa wajitokeze.
“Hadi sasa kozi imeanza vizuri lakini mahudhurio hayaridhishi kwani mpaka sasa washiriki 20 tu wamejitokeza,tumeongeza muda wa siku mbili kuanzia leo(jana) Ili yeyote yule mwenye sifa ajitokeze"alisema Zoma.
Ni wazi kuwa makocha watakaoshiriki katika kozi hiyo watakuwa na mchango mkubwa katika kuendeleza mpira wa miguu katika mkoa wa Tabora na Taifa kwa ujumla..
 Kozi hiyo itadumu kwa siku 14.

0 comments:

Post a Comment