Wednesday, 2 July 2014

Rhino Rangers imepata viongozi wapya.

Klabu ya Rhino Rangers iliyoshiriki ligi kuu Tanzania Bara msimu uliopita na sasa kushiriki ligi daraja la kwanza FDL imepata safu mpya ya viongozi.
Viongozi hao wamepatikana baada ya klabu hiyo kukutana na wadau wa soka wa mkoa wa Tabora katika uwanja wa Alli Hassan Mwinyi.
Akitangaza majina hayo katibu wa Rhino kwa sasa  Haji Kubeja ameeleza kuwa viongozi hao wamepatikana  ili kuisimamia Rhino Kwa muda ili kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kujiandaa na ligi daraja la kwanza FDL pamoja na usajili.
Viongozi hao ni pamoja na Meja Ali Ambaye atakuwa mwenyekiti huku akisaidiwa na makamu wake Kapteni Baraja,Katibu ni Haji Kubeja,katibu msaidizi atakuwa  Clerence Kambona.
Wajumbe ambao watakuwa ndani ya klabu hiyo ni pamoja na Issa Habibu,Paul Masaka,George Nyoni.
Meneja wa timu ni Ali Likongo akisaidiwa na Nicholaus Simon.
Vilevile klabu hiyo imetengeneza kamati mbalimbali kama vile kamati ya  Utawala na vifaa,kamati ya fedha,kamati ya nidhamu,kamati ya ushauri ambayo itahusisha wakuu wa vikosi mkoani Tabora,kamati ya mahusiano ambayo itahusisha raia na wanajeshi na kamati ya ufundi.
Bwana Kubeja ameeleza kuwa kuanzia alhamisi au ijumaa kocha mpya wa timu hiyo atatajwa.
Ikumbukwe kuwa Rhino ilishuka daraja kutoka ligi kuu hadi daraja la kwanza baada ya kushika mkia katika timu zote za ligi kuu Tanzania Bara.
Rhino kwa sasa inajiandaa na FDL na imekwishaanza mazoezi ila iko katika mipango ya kwenda kupiga kambi nje ya mkoa wa Tabora.





0 comments:

Post a Comment