Makubwa,Rais wa Argentina hajawahi kuangalia mchezo hata moja wa Argentina kombe la dunia.
Rais wa Argentina Cristina Fernandez jana alikiri kuwa hajawahi kuangalia mchezo hata moja wa timu ya taifa ya Argentina katika fainali za kombe la dunia hata mchezo wa fainali kitu ambacho watu wengi wamedai kuwa rais huyo amekosa uzalendo..Baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Ujerumani bao 1-0,rais Fernandez aliwapokea vijana wa Argentina katika mji mkuu wa nchi hiyo..
Hapo awali Fernandez alipewa mwaliko kutoka rais wa Brazil Dilma Rousseff ili kuhudhuria fainali na akagoma akidai kuwa anaumwa koo huku Chancellor wa Ujerumani Angela Merkel, alikuwepo katika mchezo wa fainali na pia kushangilia sana bao la Gotze.
Akiongea baada ya kuwapokea na kuwapongeza wachezaji wa Argentina Fernandez akiwa karibu na Lionel Messi na wachezaji wengine alisema kuwa yeye si mshabiki wa soka daima.
"Sijawahi kuangalia mchezo hata moja,hata juzi kwenye fainali sijawaangalia,"alisema Fernandez
Baada ya Ujerumani kushinda watu 70 walijeruhiwa usiku wa jumapili jijini Boenes Aires huku maofisa wa polisi wengi wao wakijeruhiwa na vyombo vya habari vimeeleza kuwa watu 120 jana wameeumizwa sana katika mapigano baina yao na polisi.
0 comments:
Post a Comment