Van Gaal kutua leo Manchester United.
Kocha mpya wa klabu ya Manchester United Louis van Gaal Leo hii anatarajiwa kutua Klabuni Jijini Manchester huku ikiwepo shauku kubwa ya kuleta Wachezaji wapya.Baada ya kukirejesha Kikosi cha Uholanzi kwao baada Fainali za Kombe la Dunia toka huko Brazil, Anga za Uhamisho huko Ulaya sasa zimejaa mategemeo makubwa kuwa kuanza kazi rasmi kwa Van Gaal huko Old Trafford kutashuhudia Mabingwa hao wa zamani wakiongeza Wachezaji wao wapya baada kuwaunua Anders Herrera kutoka Athletic Bilbao na Luke Shaw kutoka Southampton.
Wachezaji wapya wanaohusishwa sana Man United ni Kiungo wa Chile, Arturi Vidal, anayechezea Juventus ya Italia, Thomas Vermaelen, Nahodha wa Arsenal, na Wachezaji Watatu waliokuwepo kwenye Kikosi cha Uholanzi huko Brazil chini ya Van Gaal, Daley Blind, Bruno Martins Indi na Stefan De Vrij.
Taarifa ya Vidal imeongezeka nguvu hasa baada ya Mchezaji huyo mwenyewe kukiri anaihusudu Man United na pia sababu ya Mchezaji wa Man United, Patrice Evra kwenda Juventus, kitu ambacho kinaonekana kulainisha ujio wa Vidal huko Old Trafford.
Van Gaal aliingoza Uholanzi kukamata nafasi ya tatu kombe la dunia na alikwisha saini mkataba wa miaka mitatu wa kuitumikia Manchester United.
0 comments:
Post a Comment