Tuesday, 8 July 2014

Manchester City yaendelea kujiimarisha,kipa wa Malaga atua kwao

Klabu ya Manchester City, imethibitisha kumsajili golikipa Willy Caballero  kutoka klabu ya Malaga kwa mkataba wa miaka mitatu.
Golikipa huyo mwenye umri wa miaka 32 alisafiri kwenda jijini Manchester kwa ajili ya kukamilisha vipimo vya afya jana ili asaini mkataba huyo wenye thamani ya paundi milioni nane.
Caballero ambaye ni raia wa Argentina aliuambia mtandao wa klabu hiyo kuwa amefurahi na uhamisho huo na atajitahidi kadri awezavyo ili aweze kuisaidia timu hiyo.
City imekuwa ikitafuta kipa atakayempa changamoto mpya Joe Hart toka Costel Pantilimont alipohamia Sunderland mapema kiangazi hiki.
Huyo anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na meneja Manuel Pellegrini katika kipindi hiki baada ya kuwachukua pia Bacary Sagna na Fernando.
Caballero alishawahi kufundishwa na Mancini wakati yupo Malaga.

0 comments:

Post a Comment