Stars kuondoka kesho kwenda Mbeya.
Timu ya soka ya taifa ya Tanzania Taifa Stars inatarajiwa kuondoka kesho kwenda Tukuyu kuweka kambi nyingine, na itarejea Dar es Salaam siku tatu kabla ya mechi Ya kufuzu AFCON 2015 nchini Morocco dhidi ya Msumbiji.Taarifa ya shirikisho la soka Tanzania,TFF kupitia kwa msemaji wake Boniface Wambura imeeleza kuwa wachezaji wanaocheza nje, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya DRC na Mwinyi Kazimoto wa Al Markhiya ya Qatar,TFF imekwishazitumia barua klabu zao kuwaomba kwa ajili ya mchezo huo.
“Kama ambavyo kanuni za FIFA zinasema, wachezaji hao wanatakiwa kuwa wamefika Dar es Salaam siku tano kabla ya mechi, hivyo tunatarajia klabu hizo zitatekeleza agizo hilo,”amesema Wambura.
Wambura amesema kwamba maandalizi ya mchezo huo yanaendelea vizuri na kiingilio cha chini kitakuwa Sh. 7,000. Amesema viingilio vingine vitatajwa baadaye.
0 comments:
Post a Comment