Matokeo Kuelekea AFCON 2015,timu zilizoanzia nyumbani mambo safi,isipokuwa Tanzania.
Bao pekee la Benin limefungwa na mchezaji wa klabu ya West Bromwich Albion,Stephane Sessegnon . Alifunga bao pekee dakika ya 19 na kuwalaza Malawi 1-0 mjini Cotonou.
Mchezo ulimalizkia kwa timu zote kuwa pungufu baada ya Wachezaji Badarou Nafiou wam Benin na Mmalawi Frank Banda kulimwa kadi nyekundu katika dakika ya 84.
Timu zote zilizoanzia nyumbani zilishinda isipokuwa Tanzania ambao wametoka sare ya 2-2 na Msumbiji.
- Jumamosi
- Botswana 2-0 Guinea-Bissau
- Uganda 2-0 Mauritania
- Sierra Leone 2-0 Seychelles
- Jumapili
- Lesotho 1-0 Kenya
- Tanzania 2-2 Msumbiji
- Congo Brazzaville 2-0 Rwanda
- Benin 1-0 Malawi
Lesotho ilishinda bao 1-0 dhidi ya
Kenya mjini Maseru.
Rwanda,
ambayo iliitoa Libya katika raundi iliyopita , ilibamizwa mabao 2-0 na Congo-Brazzaville
mjini Pointe-Noire.
Mabao ya Congo yalifungwa na Cesaire Gandze pamoja na Ferebory Dore.
Michezo ya marudiano itapigwa kati ya Agosti1-3. Michezo ya AFCON 2015 Morocco itachezwa kuanzia Januari 17 hadi Februar 8 2015.
0 comments:
Post a Comment