Kocha Brazil kutajwa kesho.
Brazil inatarajiwa kumtangaza kocha wake mpya
katika mkutano na wanahabari siku ya jumanne kufuatia kujiuzulu kwa
kocha wa timu hiyo Luiz Felipe Scolari.
Scolari mwenye umri wa miaka 65 aliiongoza
Brazil katika nusu fainali za kombe la dunia ambapo timu hiyo ilipata
kichapo kibaya cha mabao 7-1 dhidi ya mabingwa wa kombe la
Dunia Ujerumani.Aliyekuwa kocha wa timu hiyo ambaye aliiongoza timu hiyo kati ya mwaka 2006 na 2011 Dunga huenda akarejea na kuchukua kazi hiyo.
Wengine wanaopgiwa debe kuchukua kazi hiyo ni kocha wa klabu ya Corinthians Tite,kocha wa klabu ya Sau Paulo Muriciy Ramalho na Vanderlei Luxembourg ambaye aliwahi kuifunza timu hiyo kutoka mwaka 1998 hadi mwaka 2000.
0 comments:
Post a Comment