Monday, 7 July 2014

Mkongwe wa Madrid afariki dunia,Perez atoa salamu za rambirambi

Di Stefano enzi za uhai wake,akifurahia tuzo ya Ronaldo
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Real Madrid Alfredo Di Stefano amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 88.

Di Steafano  alikuwa katika hali ambayo ilikuwa hairidhishi baada ya kupata mshtuko wa moyo katika mji ulio karibu na Santiago Bernabeu siku ya jumamosi, siku chache tu baada ya kuadhimisha sherehe ya siku yake ya kuzaliwa kutimiza miaka  88,amefariki baada hali yake kuwa mbaya asubuhi ya leo.
Di Stefano alianza kucheza soka akiwa na klabu ya River Plate baadaye akajiunga na  Madrid akitokea klabu iliyopo nchini Colombia, Millonarios Mwaka  1953, kabla ya hapo alikaribia kujiunga na Barcelona.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa  Argentine aliitumikia Madrid kushinda mataji 8 ya  Liga na mataji 5 ya ligi ya mabingwa kati ya 1953 na 1964.

Amefunga mabao  308 katika michezo 396 kwa upande wa Real na nabaki kuwa mfungaji bora wa pili wa Madrid nyuma ya  Raul (323).

Real Madrid wamethibitisha kifo hicho kwenye mtandao wao.
Rais wa Real Madrid, Florentino Perez, na bodi ya klabu imetoa salamu za rambirambi kwa watoto,familia na marafiki.
MAELEZO YA DI STEFANO
Jina kamili Alfredo Stéfano di Stéfano Laulhé]
Kuzaliwa 4 July 1926
Eneo alipozaliwa Buenos Aires, Argentina
Trehe ya kifo 7 July 2014 (aged 88)
Eneo alipofariki Madrid, Spain


Nafasi uwanjani Msahambuliaji
TIMU ALIZOCHEZA
Years Timu Michezo† (mabao)
1945–1951 River Plate 66 (49)
1946 Huracán (mkopo) 25 (10)
1951–1953 Millonarios 102 (90)
1953–1964 Real Madrid 282 (216)
1964–1966 Espanyol 47 (11)
Jumla
524 (376)
Timu ya taifa
1947 Argentina 6 (6)
1957–1961 Hispania 31 (23)
Timu alizofundisha
1967–1968 Elche
1969–1970 Boca Juniors
1970–1974 Valencia
1974–1974 Sporting CP
1975–1976 Rayo Vallecano
1976–1977 Castellón
1979–1980 Valencia
1981–1982 River Plate
1982–1984 Real Madrid
1985 Boca Juniors
1986–1988 Valencia
1990–1991 Real Madrid

0 comments:

Post a Comment