Origi kutua Liverpool
Chipukizi Divock Origi, aliyeng’ara akiwa na timu ya taifa ya Ubelgiji katika Kombe la Dunia, amewasili Liverpool na anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya leo (Alhamisi) kabla ya kujiunga rasmi na miamba hao wa ligi ya Uingereza.Origi alipigwa picha Jumatano akiwasili katika uwanja wao wa mazoezi wa Melwood na anatazamiwa kufanyiwa vipimo pamoja na kiungo kutoka Benfica, Lazar Markovic.
Inasemekana kuwa Liverpool watalipa klabu cha Ufaransa, Lille, pauni milioni 10 za Uingereza kwa huduma za mshambuliaji huyo mwenye asili ya Kenya.
Alipohojiwa kuhusu hatima yake nyumbani kwao Houthalen-Helchteren, Origi Ni ukweli nimepata maombi mengi kutoka vilabu kadhaa za Ulaya.
“Lakini ni lazima niwaze ni wapi ambapo nitaweza kunawiri kama mchezaji na binadamu. Mambo yatabainika wiki mbili zijazo.”
Origi alishamiri katika dimba la dunia alipochukua nafasi ya Romelu Lukaku, akifungia taifa lake bao la ushindi dhidi ya Urusi kwenye awamu ya makundi.
Ubelgiji waliondolewa katika robo fainali na Argentina.
0 comments:
Post a Comment