Thursday, 10 July 2014

Suarez ndani ya saa 24 atakuwa mali ya Barcelona,daktari kwenda kumpima akiwa Uruguay

Mchezaji nyota Luis Alberto Suarez Diaz anakamilisha dili lake la kutangazwa rasmi kuwa mchezaji wa  Barcelona  baada ya maelewano ama uhamisho wake  wa kiasi cha  £70 mil kukubaliwa jana usiku.

Maelewano hayo yamedumu kwa takribani wiki nzima baina ya vilabu viwili na atatangazwa ndani ya saa 24 kuwa mali halali ya Barcelona.
Barcelona wanafanikiwa kumdaka Suarez na wanatakiwa kutoa hela moja kwa moja baada ya Suarez kusaini mkataba mwezi disemba na Liverpool.
Inasadikiwa kuwa Suarez  atapimwa vipimo vya afya akiwa nchini kwao   Uruguay, baada ya kupewa adhabu na FIFA kwa kisa cha kumng'ata meno beki wa Italia Chiellini katika kombe la dunia,na Barca tayari imekwishamtuma daktari wake.
Kila kitu kinakwenda vema ila kilichobaki ni Suarez kutangazwa ili awe mchezaji halali wa Barcelona,imeeleza taarifa ya mtandao wa Goal.com

Barca imeamua fedha za kumuuza Alexis Sanchez kwenda  Arsenal itatumika kama sehemu ya dili hilo.
Liverpool kwa sasa wanajiimarisha zaidi na wamekaribia kabisa kuwanasa wachezaji watatu ambao ni  winga wa  Benfica  Lazar Markovic, mshambuliaji wa Lille  Divock Origi na mlinzi wa  Southampton Dejan Lovren.

0 comments:

Post a Comment