Pigo Manchester City,Negredo avunjika guu la upande wa kulia
Klabu ya Manchester City imepata pigo baada ya Mshambuliaji wake Alvaro Negredo kuthibitika kuwa amevunjika mguu wake utakaomfanya kukaa nje ya uwanja kwa miezi kadhaa.Negredo mwenye umri wa miaka 28 aliumia katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Hearts jana na kuthibitisha taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram sambamba na picha ya mguu wake wa kulia ukiwa na bandeji gumu.
Nyota huyo aliandika
kuwa anawajulisha mashabiki wake kuwa miezi michache inayokuja itakuwa
migumu kwake kutokana na kuvunjika mguu.
Hata hivyo aliwaondoa hofu
mashabiki hao kwa kuwaambia kuwa atarudi akiwa imara zaidi zaidi ya
alivyo sasa.
Taarifa zitakuwa ni mbaya kwa kocha Manuel Pellegrini
wakati City wakitaka kutetea taji lao la ligi walilonyakuwa msimu
uliopita.


0 comments:
Post a Comment