Monday, 14 July 2014

Scolari ajisalimisha mwenyewe,aomba kujiuzulu maamuzi kutolewa leo.

Kocha wa timu ya taifa ya Brazil  Luiz Felipe Scolari ameandika barua ya kujiuzulu nafasi ya ukocha na kuipeleka   kwa shirikisho la soka la Brazil (CBF) baada ya fainali za kombe la dunia kuhitimishwa katika ardhi ya Brazil hiyo jana .

Kocha huyo mwenye miaka 65 hapo awali aligoma kujiuzulu baada ya kufungwa mabao 7-1 na Ujerumani na mwishoni mwa wiki iliyopita aliwahi kusema anawaachia maamuzi hayo CBF ili kumjadili.
Hata hivyo imeeleweka kuwa  Scolari amewataarifu  CBF jana ambapo leo jumatatu  taarifa rasmi itatoka.
Brazil maarufu kama Selecao waliianza vyema mashindano lakini kadri mashindano yalivyokuwa yanafikia mwishoni walishindwa kuhimili vishindo..

Brazil walichapa Croatia katika mchezo wa ufunguzi na kwenda sare dhidi ya  Mexico. Walishinda mbele ya Cameroon na kuingia hatua ya mtoano na walifunga Chile kwa taabu  kabla ya kuwashindilia  Colombia 2-1 katika robo fainali.

Ndoto za wenyeji kutinga fainali zilizimwa na Ujerumani baada ya kudhalilishwa 7-1 kabla ya kubamizwa na Uholanzi mabao 3-0 katika kumtafuta mshindi wa tatu.

Scolari  ameiongoza  Brazil kushinda michezo  19  katika mipambano  29  baada ya mara ya pili kuifundisha timu hiyo na kubeba kombe la mabar mwaka 2013

0 comments:

Post a Comment