Thursday, 17 July 2014

Ujerumani ya kwanza viwango FIFA,Hispania ya 8,Taifa stars 106.

Mabingwa wa dunia, Ujerumani wameendelea kufaidi mafanikio yao kufuatia kampeni yao katika michuano ya Kombe la Dunia ambapo sasa wamekwea kileleni mwa orodha za Shirikisho la Soka la Dunia kwa mara ya kwanza toka kupita miaka 20.
Fainali dhidi ya Argentina ilikuwa sio kwa ajili ya taji la dunia pekee bali pia kugombea nafasi hiyo ya juu kabisa ambapo sasa taifa hilo kutoka Amerika Kusini nao wamekwea kutoka nafasi ya tano na kuwafuatia mabingwa hao.
Nafasi ya tatu ni Uholanzi,Nafasi ya nne imetwaliwa na Colombia wakifuatiwa na Ubelgiji katika nafasi ya tano huku Uruguay wakiwa katika nafasi ya sita.
Wenyeji wa michuano hiyo Brazil wao wamekaa katika nafasi ya saba wakifuatiwa na mabingwa zamani Hispania ambao wameporomoka kutoka nafasi ya kwanza kutokana na kufanya vibaya katika michuano hiyo wakati nafasi ya tisa na 10 zikishikiliwa na Uswis na Ufaransa.
Katika orodha hizo Tanzania imejitoa kimasomaso kwa kukwea kwa nafasi saba kutoka nafasi ya 113 mpaka 106 huku kwa upande wa Afrika nako kukiwa na mabadiliko kwa Algeria kuongoza kwa kuwa katika nafasi ya 24 walikufuatiwa na waliokuwa vina Ivory Coast katika nafasi ya 25.
Kumi bora duniani
1. Germany
2. Argentina
3. Netherlands
4. Colombia
5. Belgium
6. Uruguay
7. Brazil
8. Spain
9. Switzerland
10. France

0 comments:

Post a Comment