Saturday, 19 July 2014

Tutakuwa imara zaidi Msimu huu-Wenger.

Kocha  wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amesema Kikosi chake kitakuwa imara kwa Msimu ujao na wanatarajia kutwaa Makombe mengine baada Msimu uliopita kumaliza ukame wa Miaka 9 kwa kutwaa kombe la FA .
Msimu mpya wa Arsenal utaanza rasmi Uwanjani Wembley hapo Agosti 10 kwa kucheza Mechi ya kuwania Ngao ya Jamii dhidi ya Mabingwa Manchester City.
Tayari Wenger ameimarisha Kikosi chake kwa kuwaongeza Wachezaji wawili wapya, Alexis Sanchez kutoka Barcelona na Mathieu Debuchy wa Newcastle, na pia anatarajia nyota  wake Theon Walcott, alieumia vibaya Goti Mwezi Januari, kurudi Uwanjani mwishoni mwa Agosti.
Lakini Wenger anatarajia kuongeza Wachezaji wapya wengine na wanakaribia kumnasa Kipa wa Colombia, David Ospina, kutoka Klabu ya France, Nice.
Wenger amesema: “Tunayo nia, tunayo ari, tutajiamini kutokana na Msimu uliopita, hivyo tuna msingi mzuri. Sasa ni juu yetu kuhakikisha tuna mwelekeo mzuri na njaa ya kuongeza Mataji zaidi!”
Hata hivyo, Wenger ameonya kuwa Ligi Kuu England haitabiriki hasa baada ya kila Timu kujiimarisha.
Lakini Wenger amesema: “Kitu ambacho tuna uhakika na ambacho lazima tukihakikishe ni kuwa tuko tayari kupigana na kuwa bora kupita Msimu uliopita!”
Kuhusu Sanchez, Wenger amesema wamelipa Fedha nyingi kumnunua Mchezaji huyo kwa sababu ni Mchezaji mzuri anayeweza kucheza Winga zote, katikati na ana ubora unaohitajika Uingereza.
Kwa upande wa majeruhi Theo Walcoott, Wenger amesema Mchezaji huyo anaendelea vyema baada kuumia vibaya Goti Mwezi Januari na ataanza Mazoezi kamili mwishoni mwa Agosti.

0 comments:

Post a Comment