Wanaowania tuzo za kombe la dunia 2014 Kwenye picha tofauti.
Shirikisho la soka duniani FIFA imetangaza Majina ya Wachezaji 10 watakaogombea Tuzo ya Mchezaji Bora wa Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil, Tuzo ya Mpira wa Dhahabu.Listi hiyo ya Wachezaji 10 inao Wachezaji Wanne kutoka Ujerumani, Watatu wa Argentina huku Colombia, Brazil na Uholanzi zikitoa Mchezaji mmpja moja.
Wachezaji wa Argentina ambao wako kwenye Lisi hiyo ni Angel Di Maria, Javier Mascherano na Lionel Messi.
Ujerumani ni Mats Hummels, Toni Kroos, Phillip Lahm na Thomas Muller.
Waliobaki ni Straika wa Colombia James Rodriguez, Nyota wa Brazil Neymar na Arjen Robben wa Uholanzi.
‘GLOVU YA DHAHABU’
Vile vile FIFA imateja Majina ya Makipa Watatu ambao watawania Tuzo ya Kipa Bora wa Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil.
![]() |
Manuel Neur |
Makipa hao ni Kipa wa Costa Rica Keylor Navas, Manuel Neuer wa Germany na Kipa wa Argentina Sergio Romero.
‘MCHEZAJI BORA KIJANA’
Pia, mshambuliaji wa Uholanzi Memphis Depay pamoja na Paul Pogba na Raphael Varane wa Ufaransa wameteuliwa kugombea Tuzo ya Mchezaji Bora Kijana.
![]() |
Depay Memphis |

Angel Di Maria akishangilia bao la ushindi Argentina ikishinda kwa Uswisi

Arjen Robben akishangilia ushindi wa 5-1 dhidi ya Hispania

James Rodriguez AMEFUNGA MABAO 6

Thomas Muller alifunga hat-trick dhidi ya Portugal

Ujerumani iliposhinda 7-1 dhidi ya Brazil

Toni Kroos akishangilia bao la tatu dhidi ya Brazil

Mats Hummels akishangilia bao dhidi ya Ufaransa

Ochoa naye alijitahidi lakini hayupo kwenye list
0 comments:
Post a Comment