Manchester United yauza tiketi zote 55,000 Msimu mzima Old Traford
Klabu ya Manchester United imetangaza kuwa Tiketi
zote 55,000 za kuingia kwenye Mechi katika Uwanja wa Old Trafford kwa Msimu
mzima zimeuzwa na hii imevunja Rekodi ya Tiketi za Msimu kumalizika
mapema.
Wachambuzi
wanadai kuuzwa huko kwa Tiketi hizo haraka tangu Old Trafford
ilipopanuliwa na kuwa ya Viti 76,000 Mwaka 2006 kumekuja hasa kutokana
na shauku ya Mashabiki baada ya kocha wao mpya Louis van Gaal kufanya
vizuri huko Brazil akiwa na Uholanzi na kuifikisha Nusu Fainali ya
Kombe la Dunia.
Baada kuuzwa Tiketi hizo 55,000 Tiketi
zilizobaki 21,000 huwekwa pembeni kwa makusudi na rasmi kwa ajili ya
Mashabiki wa Timu za Ugenini na kwa Mashabiki wanaotaka kuhudhuria
baadhi ya Mechi na si Mechi zote za Msimu wote.
Watu wengi walihofia kuwa baada ya Man
United kufanya vibaya Msimu uliopita chini ya David Moyes na kumaliza
Ligi wakiwa Nafasi ya 7 na hivyo kukosa kabisa kucheza Mashindano ya
Klabu Ulaya kungeweza kuathiri mahudhurio ya Watazamaji Old Trafford.
Lakini hali imekuwa tofauti hasa baada
ya kumtangaza Louis van Gaal kocha mpya ambaye anatarajiwa kutambulishwa
rasmi huko Old Trafford Alhamisi kabla Ijumaa kuruka kwenda Marekani
kwa Ziara Kabla Msimu Mpya Kuanza.
Hivi sasa Kikosi cha Man United, bila ya
Wachezaji walioshiriki Kombe la Dunia huko Brazil na Nchi zao, kimeanza
Mazoezi chini ya Ryan Giggs huko Jijini Manchester kwenye Kituo chao
cha Mazoezi cha AON Training Complex.
Man United wataruka hapo Ijumaa Julai 18
kuelekea huko Marekani na kupiga Kambi huko California kabla ya kucheza
Mechi yao ya Kwanza huko USA hapo Julai 23 dhidi ya LA Galaxy kugombea
Chevrolet Cup ndani ya Rose Bowl, Pasadena.
0 comments:
Post a Comment